FURSA ZA MASOMO: UFADHILI WA MASOMO NCHINI JAPAN.

Location:
Date Posted: May 11, 2023
Application deadline: Jun 5, 2023

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuujulisha umma kuhusu uwepo wa fursa za ufadhili wa masomo zinazotolewa na Serikali ya Japan kupitia Wizara ya Elimu, Utamaduni, Michezo, Sayansi na Teknolojia (Ministry of Education, Culture, Sports, Science and Technology - MEXT) kwa mwaka wa masomo 2024.

Ngazi ya masomo

  1. Shahada ya Kwanza (Undergraduate Studies).
  2. Umahiri (Master’s Degree).
  3. Uzamivu (PhD.)
  4. Mafunzo ya ufundi (Specialized Training College).

Mwisho wa Kutuma Maombi

  • 05 Juni 2023 saa 10.30 Jioni.

Maombi yote yapitie Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.

Kwa taarifa zaidi https://rb.gy/bzqwt