Vyuo na Vyuo Vikuu ni kitengo kimojawapo kilichopo kwenye Idara ya Uhusiano wa Kimataifa , Vyuo na Vyuo Vikuu ambayo ni miongoni mwa Idara nne (4) zinazounda Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Kitengo hichi kinasimamia na kuratibu shughuli zote za wanafunzi wa vyuo na vikuu, kuandaa na kutoa mafunzo ya itikadi, semina, makongamano, matamasha na warsha mbalimbali.
Kushughulikia Uratibu wa masuala ya wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu kupitia Matawi yao ambayo lazima yawe nje ya maeneo ya Vyuo.
Kusimamia na kufuatilia harakati za kisiasa na za kitaaluma za wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu.
Kuwa kiungo kati ya Vyuo na Vyuo Vikuu na Vikao vya Jumuiya na chama katika ngazi zote.
Kuzimamia shughuli za uchaguzi wa viongozi wa Vyuo na Vyuo Vikuu, na uchaguzi wa uwakilishi kupitia vyombo vya dola.
Kusajili wanafunzi katika matawi ya Vyuo na Vyuo Vikuu kwa sabaha ya kuwa na wanachama kwa kadiri inavyowezekana.
Kushiriki mikutano, midahalo na makongamano kwa ajili ya kuwajenga wanavyuo wawe na uwezo wa kujiamini kuhusu nchi yao na nafasi ya Chama cha Mapinduzi.
Kuwajenga wanafunzi katika maadili ya uzalendo, umoja na utaifa. Pia kuthubutu kutenda katika mazingira ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Kuunga mkono na kushiriki kikamilifu katika ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na taaluma za wasomi kwa lengo la kuimarisha moyo wa uvumbuzi miongoni mwa jamii ya vijana wasomi wa Taifa.
Kukuza uhusiano na ushirikiano baina ya Vyuo na Vyuo Vikuu na Taasisi za hiari zinazojishughulisha na masuala ya elimu, sayansi na utamaduni ndani na nje ya Tanzania.