UFADHILI WA MAFUNZO STADI KWA VIJANA WENYE ULEMAVU.

Location:
Date Posted: Apr 10, 2023
Application deadline: Apr 10, 2023

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetoa fursa ya ufadhili kwa ajili ya vijana 92 wenye ulemavu kupata mafunzo ya ufundi stadi.

Mahali: Chuo cha Ufundi kwa Watu wenye Ulemavu Sabasaba - Singida.

Kuripoti: 12 Aprili 2023.

Fani zitakazotolewa:

 1. Ushonaji nguo.
 2. Useremala.
 3. Ufundi simu.
 4. Uokaji keki na mikate.
 5. Umeme wa majumbani.
 6. Uchomeleaji.
 7. Ususi na urembo.

Umri: Miaka 15 - 40.

Aina ya ulemavu: Ulemavu wa aina zote na mwombaji awe na uwezo wa kujihudumia kama kula n.k.

Muda wa Mafunzo: Miezi 3.

Ufadhili Unahusisha:

 1. Mafunzo.
 2. Malazi.
 3. Chakula.
 4. Posho ya kujikimu.
 5. Nauli ya kwenda na kurudi chuoni.

 Mawasiliano:

Wasiliana na uongozi wa chuo kwa ajili ya fomu na taratibu za kujiunga.

Mratibu wa Mafunzo: 0755 261 127.

Mkuu wa Chuo: 0753 032 727.


#JisajiliSasa

#VyuoNaVyuoVikuu

#UkomboziWaFikiraNaHali


Download