TANGAZO LA MAOMBI YA MAFUNZO YA KILIMO KWA VIJANA.

Location:
Date Posted: Jan 19, 2023
Application deadline: Jan 30, 2023

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza Programu ya Kuwezesha Ushiriki wa Vijana katika Kilimo Biashara (Building a Better Tomorrow Youth Initiative for Agribusiness (BBT-YIA). Programu hii inatarajiwa kuongeza ajira kwa vijana kufikia milioni tatu (3) na kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo hadi kufikia asilimia10 ifikapo mwaka 2030 (Ajenda 10/30).

Kupitia BBT, Wizara inaratibu uanzishwaji wa mashamba makubwa ya pamoja (Block Farms) kwa ajili ya vijana. Mradi huu utatekelezwa nchi nzima na vijana wote wenye sifa watapata fursa ya kufanya kilimo biashara katika mnyororo wa thamani. Kwa kuanzia, Wizara imetambua mashamba yenye jumla ya ekari 162,492 katika Wilaya ya Chunya (Mbeya); Bahi na Chamwino (Dodoma); na Misenyi na Karagwe (Kagera); na Uvinza na Kasulu (Kigoma).

Wizara inatangaza fursa za mafunzo ya kilimo biashara kwa awamu ya kwanza kwa vijana katika Kituo cha Mafunzo ya Kilimo Bihawana mkoani Dodoma. Mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 15 Februari 2023 ambapo vijana watapatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu. Baada ya mafunzo hayo, wahitimu watakabidhiwa mashamba kwa ajili ya kilimo kwa taratibu na masharti yatakayoainishwa.

Maombi yote yatumwe kupitia kiunganishi cha bbt.kilimo.go.tz kuanzia leo tarehe 10 Januari, 2023.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Januari 2023.

Sifa za vijana wanaotakiwa kuomba ni pamoja na:-

  1. Awe Mtanzania.
  2. Awe na umri kati ya miaka 18 - 40.
  3. Awe anapenda kufanya kilimo biashara; na iv. Awe anashiriki kwenye shughuli za kilimo. 

Download