TAMISEMI: TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA NA ELIMU.

Location:
Date Posted: Apr 21, 2022
Application deadline: May 4, 2022

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) imepata kibali cha ajira za Watumishi wa Kada za Afya 7,612 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Ualimu 9,800 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 20 Aprili - 04 Mei, 2022.

Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree). 

A: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA ZA UALIMU.

Walimu wote wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz

Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2021. Waombaji ambao waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo wa maombi ya ajira wanatakiwa kuomba upya.

B: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA KADA ZA AFYA.

Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha  ajira.tamisemi.go.tz

Waombaji ambao waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo wa maombi ya ajira wanatakiwa kuomba upya.


Download